Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Kilimo na Mifugo (TRACDI) anapenda kuwatangazia watu wote kuwa tayari wameanza kupokea maombi ya kujiunga na masomo katika ngazi zote kwa muhula wa mwezi Tisa kwa mwaka wa masomo wa 2019/2020 kuanzia tarehe 15 Mei, 2019.

Fomu za maombi ya kujiunga na masomo zinapatikana chuoni na kwenye tovuti ya chuo. Chuo kina mazingira mazuri na rafiki ya kusomea na miundombinu ya kutosha. Huduma ya Hosteli ni BURE kwa wanafunzi wote.

Pia maombi ya kujiunga yanaweza kufanyika kupitia mfumo wa mtandao uliopo kwenye tovuti ya chuo kwa kubofya kitufe cha APPLY ONLINE

Kwa maelezo zaidi tafadhali usisite kutupigia kupitia namba zifuatazo:- 0786829290, 0765970455, 0769479835

KARIBU SANA

June 4th, 2019