KUFUNGULIWA KWA UDAHILI KWA MUHULA MPYA WA MASOMO WA MWEIZ TISA 2022
Ofisi
ya Mkuu wa chuo TRACDI inapenda kuwaarifu wazazi ,walezi na wanafunzi
kuwa Baraza la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi NACTVET limefungua rasmi dirisha la maombi ya kujiunga na masomo kwa ngazi ya Certificate na Diploma kwa muhula utakaonza mwezi wa kumi.
Mkuu wa chuo anapenda kuwakumbusha kuwa chuo kinatoa mafunzo katika kozi za
Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya Certificate na Diploma.
Pia chuo kinatoa Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji kwa ngazi ya VETA kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwa ufaulu wowote.
Masomo yataanza tarehe 10/10/2022
Chuo
kitakuwa na mafunzo maalumu kwa wanafunzi kama vile Kuendesha
Trekta,mafunzo ya namna bora ya ufugaji na uangulishaji wa vifaranga na
uendeshaji wa mashine za kutotoleshea Incubator pamoja mafunzo karibishi
orientation
Hivyo wanafunzi wote watakaoomba nafasi wanashauriwa kuripoti mapema chuoni kuanzia mwezi wa Tisa.
Maombi
yanapokelewa kuanzia sasa,amombi yanafanyika kupitia Website ya chuo
www.tracdi.ac.tz/apply online au fika chuoni moja kwa moja eneo la
Nzuguni.
Nyote mnakaribishwa
May 17th, 2022