Ofisi ya Mkuu wa chuo TRACDI inapenda kuwaarifu wazazi ,walezi na wanafunzi kuwa Baraza la Elimu ya Ufundi NACTE wamefungua dirisha la udahili kwa muhula mpya wa Masomo kwa mwezi wa Tisa.
Hivyo tunapenda kuwajulisha kuwa Chuo cha TRACDI Dodoma tumeanza kupokea maombi ya wanafunzi kujiunga na chuo Chetu kinachotoa mafunzo katika kozi za Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya Certificate na Diploma.
Pia chuo kinatoa Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji kwa ngazi ya VETA kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwa ufaulu wowote.
Chuo kitakuwa na mafunzo maalumu kwa wanafunzi kama vile Kuendesha Trekta,mafunzo ya namna bora ya ufugaji na uangulishaji wa vifaranga na uendeshaji wa mashine za kutotoleshea Incubator pamoja mafunzo karibishi orientation
Hivyo wanafunzi wote watakaoomba nafasi wanashauriwa kuripoti mapema chuoni kuanzia mwezi wa Nane.
Maombi yanapokelewa kuanzia sasa,amombi yanafanyika kupitia Website ya chuo www.tracdi.ac.tz/apply online au fika chuoni moja kwa moja eneo la Nzuguni.
                                              Nyote mnakaribishwa

May 17th, 2021