TANGAZO KWA WANAFUNZI WOTE.

Uongozi wa chuo (TRACDI) unapenda kuwataarifu wanafunzi wote juu ya tamko la Mh.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,John Pombe Magufuli kuhusu kufunguliwa vyuo vyote nchini Tarehe 01/06/2020.

Kwa tangazo hilo uongozi unapenda kuwajulisha wanafunzi wote kwamba wanatakiwa kuripoti mapema chuoni ili kukamilisha zoezi la usajili na kuanza masomo haraka iwezekanavyo.Pia tunawakumbusha ya kwamba usajili ni pamoja na ulipaji wa ada,hivyo kila mwanafunzi anatakiwa kufanya malipo ya ada benki kabla ya kuripoti chuoni kwa usajili.

Uongozi wa chuo unapenda kuwajulisha pia ya kuwa muhula utakwenda haraka ili kuweza kufidia muda ambao masomo yalikuwa yamesimama ili kutoathiri ratiba ya muhula wa mwezi wa tisa kama vile ambavyo NACTE wamevieleza vyuo vyote kufanya hivyo wanafunzi wote mnatakiwa kuzingatia kuripoti mapema.
Pia chuo kinapenda kuwapongezeni kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya juu ya kujilinda na maambukizi ya COVID 19 kikiamiani kuwa sote tupo salama wakati huo huo tukiendelea kuchukua tahadhari ili tuendelee kuwa salama.

Kwa wanafunzi waliokuwa wanatarajia kuanza masomo mwezi wa tatu kwa March intake 2020/2021 pia wanatakiwa kuanza kuripoti chuoni mapema kuanzia tarehe 01/06/2020 kwa ajili ya usajili.

Uongozi wa chuo unawakaribisheni wote Karibuni (TRACDI)

May 25th, 2020