Kufunguliwa kwa Dirisha la udahili kwa muhula mpya wa masomo 2020/2021.

Ofisi ya mkuu wa chuo TRACDI inapenda kuwataarifu wazazi, walezi pamoja na wahitimu wa kidato cha nne wote kuwa dirisha la udahili kwa muhula mpya wa masomo utakaoanza tarehe 16/11/2020 limefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15/06/2020 mpaka tarehe 15/09/2020.

Hivyo waombaji wote wanashauriwa kufanya maombi kuanzia sasa kupitia website ya chuo www.tracdi.ac.tz kwa kufungua link iliyopo katika website ya chuo (apply online au kwa kudownload fomu)

Pia unaweza kufika chuoni moja kwa moja, Chuo kipo katika jiji la Dodoma karibu na stend mpya ya mkoa eneo la Nzuguni

Nyote mnakaribishwa

 

June 18th, 2020