KUFUNGULIWA DIRISHA UDAHILI WA MKUPUO WA MWEZI WA TISA 2022/2023

KUFUNGULIWA KWA UDAHILI KWA MUHULA MPYA WA MASOMO WA MWEIZ TISA 2022

Ofisi ya Mkuu wa chuo TRACDI inapenda kuwaarifu wazazi ,walezi na wanafunzi kuwa Baraza la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi NACTVET limefungua rasmi dirisha la maombi ya kujiunga na  masomo kwa ngazi ya Certificate na Diploma kwa muhula utakaonza mwezi wa kumi.

Mkuu wa chuo anapenda kuwakumbusha kuwa chuo kinatoa  mafunzo katika kozi za Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya Certificate na Diploma.

Pia chuo kinatoa Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji kwa ngazi ya VETA kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwa ufaulu wowote.

Masomo yataanza tarehe 10/10/2022
Chuo kitakuwa na mafunzo maalumu kwa wanafunzi kama vile Kuendesha Trekta,mafunzo ya namna bora ya ufugaji na uangulishaji wa vifaranga na uendeshaji wa mashine za kutotoleshea Incubator pamoja mafunzo karibishi orientation
Hivyo wanafunzi wote watakaoomba nafasi wanashauriwa kuripoti mapema chuoni kuanzia mwezi wa Tisa.
Maombi yanapokelewa kuanzia sasa,amombi yanafanyika kupitia Website ya chuo www.tracdi.ac.tz/apply online au fika chuoni moja kwa moja eneo la Nzuguni.
                                              Nyote mnakaribishwa