KUFUNGULIWA KWA UDAHILI KWA MUHULA MPYA WA MASOMO WA MWEZI WA TISA 2023/2024

Ofisi ya Mkuu wa chuo TRACDI inapenda kuwaarifu wazazi ,walezi na wanafunzi kuwa Baraza la Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi NACTVET limefungua rasmi dirisha la maombi ya kujiunga na  masomo kwa ngazi ya Certificate na Diploma kwa muhula utakaonza mwezi wa Tisa 2023.

 Mkuu wa chuo anapenda kuwakumbusha kuwa chuo kinatoa  mafunzo katika kozi za Kilimo,Mifugo na Maendeleo ya Jamii kwa ngazi ya Certificate na Diploma.

 Kwa Muhula wa mwezi wa Tisa chuo kinadahili katika kozi za Maendeleo ya Jamii,Kilimo pamoja na kozi ya Mifugo.

 Pia chuo kinatoa Mafunzo ya Kilimo na Ufugaji kwa ngazi ya VETA kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kwa ufaulu usiopungua masomo mawili.

 Unaweza kufanya mamombi kwa Kudaunlodi Fomu kwa kubonyeza Link ya Application kwenye website ya chuo au kupitia Online Application.

 Masomo yataanza mwezi wa Tisa mwishoni

Chuo kitakuwa na mafunzo maalumu kwa wanafunzi kama vile Kuendesha Trekta,mafunzo ya namna bora ya ufugaji wa kisasa pamoja mafunzo ya ujasiliamali.

 Hivyo wanafunzi wote watakaoomba nafasi wanashauriwa kuripoti mapema chuoni kuanzia tarehe 15/09/2023.

 Maombi yanapokelewa kuanzia sasa,amombi yanafanyika kupitia Website ya chuo www.tracdi.ac.tz/apply online au fika chuoni   moja kwa moja eneo la Nzuguni.

  Nyote mnakaribishwa